BERLIN: Leo ni siku ya Malaria duniani
25 Aprili 2007Matangazo
Ujerumani imetoa mwito juu ya kuimarisha juhudi katika harakati za kupambana na maradhi ya Malaria yanayowauwa watu milioni moja na laki mbili kila mwaka na idadi kubwa ikiwa ni barani Afrika.
Serikali ya Ujerumani imetoa mwito huo katika maadhimisho ya siku ya Malaria inayoadhimishwa kote duniani leo hii.
Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani bibi Heidemarie Wieczorek-Zuel amesema kuwa Ujerumani itaendelea kuunga mkono mfuko wa dunia wa kupiga vita magonjwa ya Kifua Kikuu, Ukimwi na Malaria.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezitaka nchi tajiri duniani zitekeleze ahadi ilizotoa juu ya kuzisaidia nchi masikini.