1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kurnaz alikuwa kitisho kwa usalama

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEO

Aliekuwa waziri wa ndani wa Ujerumani,Otto Schily ametoa ushahidi wake mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kesi ya Murat Kurnaz,Mturuki aliezaliwa Ujerumani ambae alizuiliwa Guantanamo Bay hadi mwaka jana.Schily amechukua dhamana ya kisiasa kuhusika na kesi hiyo.Amesema,ni wizara ya ndani na si ofisi ya Kansela wala wizara ya mambo ya kigeni zilizokuwa na dhamana ya kutathmini ikiwa usalama ulihatarishwa.Amesema, Kurnaz alikuwa kitisho kwa usalama na kwa sababu hiyo ikaamuliwa kuwa arejeshwe Uturuki badala ya Ujerumani.Schily akaongezea kuwa hatua iliyochukuliwa na wizara yake kuhusika na Kurnaz ni barabara na hakuna sababu ya kutia mashakani maamuzi yaliyopitishwa na idara ya upelelezi ya Ujerumani BND na idara ya upelelezi wa uhalifu. Kurnaz alikamtwa nchini Pakistan mwaka 2001 akishukiwa kuwa ni gaidi na alizuiliwa katika jela ya jeshi la Marekani Guantanamo Bay kwa zaidi ya miaka minne.