1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kitisho cha mashambulizi ya kigaidi nchini Ujerumani

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpM

Waziri wa masuala ya ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble ameonya kuwa Ujerumani inakabiliwa na kitisho cha mashambulizi ya kigaidi.

Wakati huo huo,katibu wa nchi katika wizara ya ndani,August Hanning amesema,kuna ishara kuwa kuna harakati mpya.Akieleza juu ya mashambulizi ya kujitolea muhanga nchini Afghanistan alisema, mashambulizi ya kujitolea muhanga yanazidi kushuhudiwa nchini humo.Akaongezea kuwa Wajerumani na taasisi za Kijerumani zinalengwa nchini Afghanistan.Na kinachotia wasiwasi ni kuona uwezo wa Al-Qaeda ukiongezeka.

Kwa upande mwingine,mkuu wa idara ya polisi wa kupambana na uhalifu,nchini Ujerumani,Jörg Ziercke amesema,Wajerumani 3 wa Kiislamu wamekamatwa nchini Pakistan,wakiwa na lengo la kufanya ugaidi nchini Ujerumani.Amesema,watu hao ni miongoni mwa kundi la Waislamu 10 wa Kijerumani waliopewa mafunzo na wanamgambo wa Kitaliban,kwa azma ya kufanya mashambulizi ya bomu ya kujitolea muhanga,nchini Ujerumani na vile vile dhidi ya vikosi vya Kijerumani nchini Afghanistan.Ziercke amesema,wanaume hao ni Wajerumani walioslimu na hufuata msimamo mkali.Hatua za kuimarisha usalama na ukaguzi mipakani,zimechukuliwa na serikali ya Ujerumani.