1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kikosi maalum kupambana na uhalifu wa mpango

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTj

Ujerumani na Italia zimekubali kuunda kikosi cha pamoja kusaidia juhudi za kupambana na uhalifu wa mpango,unaofanywa na makundi ya Kitaliana.Mkuu wa Idara ya Ujerumani kuhusu masuala ya uhalifu, Joerg Ziercke amesema,lengo la kikosi hicho maalum ni kufichua uhusiano wa koo za Kitaliana na jamaa wa familia zao,nchini Ujerumani na vile vile kuimarisha utaratibu wa kubadilishana habari.

Tarehe 15 mwezi wa Agosti,Wataliana 6 walipigwa risasi na kuuawa katika mji wa Duisburg nchini Ujerumani.Inaaminiwa kuwa mauaji hayo yanahusika na ugomvi wa miaka mingi,kati ya familia za koo mbili halifu,zinazotoka eneo la Calabria,nchini Italia.