BERLIN: Kesi mpya za homa ya mafua ya ndege
6 Julai 2007Matangazo
Wataalamu nchini Ujerumani na Ufaransa wanaimarisha hatua za kinga dhidi ya homa ya mafua ya ndege.Hatua hizo zimechukuliwa baada ya maafisa wa Kijerumani kuripoti kesi 38 mpya katika jimbo la Saxony-Anhalt,ikihofiwa kuwa zinahusika na virusi vya H5N1.Tangu mwisho wa mwezi uliopita,Saxony-Anhalt ni jimbo la nne kutoka majimbo 16 ya Ujerumani kuripoti homa ya mafua ya ndege.