1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela wa Ujerumani atetea sera za serikali

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQS

Nchini Ujerumani,upinzani umeituhumu serikali ya mseto ya Kansela Angela Merkel,kuwa haiwaruhusu Wajerumani kunufaika vya kutosha kutokana na uchumi ulioimarika hivi sasa nchini humu.Mdahalo wa bajeti ya serikali ya mwaka 2008 ukiendelea kwa siku ya pili mjini Berlin,chama cha Liberali kimesema,kodi inapaswa kupunguzwa ili uwekezaji wa binafsi upate kupigwa jeki.Kansela Merkel amekanusha tuhuma zilizotolewa na akaeleza kuwa tangu aliposhika madaraka miaka miwili iliyopita, idadi ya wakosa ajira imepunguka kwa zaidi ya milioni moja.Amesema,hayo ni maendeleo mazuri mno na amekariri lengo la serikali yake kupunguza zaidi,idadi ya wakosa ajira.