1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela Merkel wa Ujerumani aizuru India

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BY

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel hii leo anaanza ziara yake ya kwanza nchini India.Mada yake kuu wakati wa ziara hiyo ya siku nne katika mji mkuu wa India,New Delhi na mji wa biashara Mumbai ni kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na sayansi kati ya Ujerumani na India.

Kansela Merkel amefutana na ujumbe wa wafanya biashara,wakiwemo mameneja wa makampuni ya Siemens,BASF na shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn.Ujumbe huo pia una wanasayansi na maafisa wa mashirika ya misaada.Mabadiliko ya hali ya hewa duniani ni mada itakayojadiliwa pia na Kansela Merkel atakapokutana na Waziri Mkuu wa India,Manmohan Singh.