BERLIN: Kansela Merkel kuhudhuria misa ya kumbukumbu
18 Agosti 2007Matangazo
Misa ya kumbukumbu ya polisi watatu wa Kijerumani waliouawa nchini Afghanistan,itasomwa hii leo Jumamosi katika Kanisa Kuu mjini Berlin.Kansela Angela Merkel atahudhuria misa hiyo.Hapo awali, ndege ya jeshi la Ujerumani-Bundeswehr ikiwa na maiti za polisi hao watatu,itapokewa na maafisa na familia za marehemu katika uwanja wa ndege wa Berlin.
Polisi hao waliuawa siku ya Jumatano katika shambulizi la bomu lililotegwa kando ya barabara katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul.