1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Kansela Merkel ataka jeshi la Ulaya

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG5

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kuundwa kwa jeshi la Ulaya inabidi liwe mojawapo ya malengo makuu ya Umoja wa Ulaya katika miaka inayokuja pamoja na suala la kuifufuwa katiba ya umoja huo iliokwama.

Kansela Merkel alikuwa akizungumza kabla ya mkutano wa mwishoni mwa juma wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Berlin kuadhimisha miaka 50 ya Mkataba wa Rome.

Mkataba huo ndio ulioanzisha msingi ambao hatimae umekuja kuunda kile kinachojulikana leo hii kama Umoja wa Ulaya.