1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela Merkel ameridhika na ziara ya India

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ad

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amerejea Berlin baada ya kukamilisha ziara yake ya kwanza nchini India.Wakati wa ziara hiyo ya siku nne, yamepatikana makubaliano ya kuzidisha maradufu kiwango cha biashara kati ya Ujerumani na India katika kipindi cha miaka mitano.

Kwa maoni ya Kansela Merkel,ziara yake nchini India imepiga jeki uhusiano wa Ujerumani na India katika sekta mbali mbali kama kuimarishwa mawasiliano ya kisiasa,uwezo wa kushirikiana kiuchumi na kuendeleza ushirikiano.

Mwishoni mwa ziara yake,Kansela wa Ujerumani alisisitiza kuwa India ni mshirika muhimu wa kisiasa barani Asia.