BERLIN: Kansela Merkel ameanza ziara ya Mashariki ya Kati
31 Machi 2007Matangazo
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo anaanza ziara yake ya siku tatu katika Mashariki ya Kati.Kituo cha kwanza cha ziara hiyo ni Aqaba nchini Jordan ambako atakutana na Mfalme Abdallah wa Pili kuchunguza juhudi za kufufua majadiliano ya amani kati ya Israel na Wapalestina.Vile vile wataujadili mpango wa amani ulioidhinishwa upya na viongozi wa nchi za Kiarabu hivi karibuni katika mkutano wao mjini Riyadh.Baada ya kuonana na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan,Kansela Merkel atakwenda Israel,Maeneo yanayotawalwa na Wapalestina na Lebanon.Merkel ambae hivi sasa ameshika wadhifa wa urais katika Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita,atawatembelea pia wanamaji wa Kijerumani nchini Lebanon.