BERLIN: Kansela Merkel ameahidi kuunga mkono mpango kuhusu Kosovo
18 Julai 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ameahidi kuunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kosovo.Merkel alitamka hayo alipokutana na Waziri Mkuu wa Serbia Vojislav Kostunica mjini Berlin. Wakati huo huo,mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana amesema,majadiliano kuhusu Kosovo yanaweza kufanywa nje ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Urusi imetishia kutumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama ili kuzuia jimbo la Kosovo kujitenga na Serbia iliyo mshirika wa Moscow.Kwa upande mwingine,viongozi wenye asili ya Kialbania katika jimbo la Kosovo lililojitenga na Serbia wanasema,Baraza la Usalama limeshindwa kuleta maafikiano na wameziomba nchi za Magharibi zitafute njia nyingine ya kulipatia jimbo hilo uhuru wake.