BERLIN: Kansela Merkel akaribisha azimio la Lebanon
12 Agosti 2006Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amefurahia hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kuidhinisha azimio la Lebanon.Amesema hiyo ni ishara muhimu ya azma ya umoja huo kumaliza mapigano.Serikali ya Ujerumani daima imejitahidi kutafuta suluhisho la kidiplomasia kuhusika na mgogoro huo.Kutoka Berlin Kansela Merkel amesema, sasa azimio hilo litekelezwa kwa haraka.