Berlin. Kansela kwenda China leo.
26 Agosti 2007Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema jana Jumamosi kuwa atajadili suala la Darfur pamoja na haki za binadamu nchini China na viongozi mjini Beijing wakati wa ziara yake katika bara la Asia.
Merkel amesema kuwa Ujerumani na China zimekuwa na uhusiano wa karibu sana na wanaweza kujadili masuala hayo.
Merkel anaondoka leo Jumapili na atakuwa nchini China hadi Jumatano kwa mazungumzo na rais Hu Jintao na waziri mkuu Jiabao.
Na baadaye atakwenda nchini Jipan kwa ziara yake ya kwanza , ambapo atakutana na mfalme Akihito na waziri mkuu Shinzo Abe katika ziara ya siku tatu nchini humo.
China ambayo ni muwekezaji mkubwa nchini Sudan na kununua kiasi cha theluthi mbili ya mafuta yanayozalishwa nchini humo, imekuwa ikipata mbinyo kutumia nafasi yake hiyo kuishinikiza serikali ya Khartoum linapokuja suala la mzozo wa jimbo la Darfur.