1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amewatolea mwito raia ...

31 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFnT

wayakubali mageuzi yatakayoanza kufanya kazi kuanzia kesho january mosi na kuchangia kwa namna hiyo kuifanya Ujerumani iwe ya kimambo leo.Kutokana na kupungua kodi za mapato kuanzia kesho,uchumi wa Ujerumani utanawiri-na dalili za hali zimeshaanza kuchomoza-amesema kansela Gerhard Schröder katika hotuba yake ya mwaka mpya itakayotangazwa na televisheni za humu nchini hii leo.Amesisitiza raia wanawajibika kwa sehemu kubwa kuamua hatima ya ukuaji wa kiuchumi wa nchi hii.Kansela gerhard Schröder amekiri hata hivyo mageuzi yatakayoanza kufanya kazi kuanzia kesho yatawafanya baadhi ya raia wazidi kufunga mikaja.Kansela Gerhard Schröder amesifu michango ya Ujerumani katika kutatua mizozo ya kimataifa-akiyataja pia maafa ya kimaumbile yaliyopita Iran hivi karibuni.Amesisitiza kataika daraja ya kimataifa Ujerumani itaendelea kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na kuwajibika zaidi Umoja wa mataifa.