Berlin: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amehakikisha serikali yake ...
16 Januari 2004Matangazo
haifikirii kubadilisha mkondo wa siasa yake kuelekea Iraq.Kansela Gerhard Schröder amesisitiza jeshi la shirikisho Bundeswehr halitoshiriki katika harakati za kijeshi nchini Iraq.Wakati huo huo ameelezea utayarifu wa Ujerumani kusaidia katika huduma za jamii.Amezungumzia uwezekano wa kutumiwa madege ya Ujerumani chapa Lazareth kusafirishia majeruhi ,wahanga wa mashambulio nchini Iraq.Mjadala kuhusu kutumwa wanajeshi wa Ujerumani nchini Iraq umepamba moto humu nchini.