1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Kansela Gerhard Schröder anasema licha ya mashambulio...

27 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxZ
ya kigaidi ya hivi karibuni mjini Instanbul,hakuna kitakachobadilishwa katika utaratibu wa kujiunga Uturuki na Umoja wa ulaya.Katika mjadala bungeni mjini Berlin,kansela Gerhard Schröder amesema Uturuki ikijiunga na Umoja wa ulaya itakua pia kwa masilahi ya usalama wa Ujerumani na Ulaya kwa jumla.Kwa maoni ya kiongozi huyo wa chama cha Social Democratic "litakua jambo la maana kabisa ikiwa Uturuki itafanikiwa kuleta uwiano kati ya Uislam na maadili ya ulimwengu huria.Waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer amepinga mapendekezo ya upande wa upinzani wa CDU/CSU,unaotaka Uturuki ipatiwe aina maalum ya ushirikiano ndani ya umoja wa ulaya badala ya kukubaliwa uanachama."Uturuki tokea hapo haitozikubali kanuni hizo,amesema waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer.