1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Jeshi la Ujerumani latakiwa kujitayarisha kwa kazi ngumu zaidi ya kulinda amani nchini Afghanistan.

18 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLu

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck ameliambia jeshi la ulinzi kujitayarisha kwa ujumbe wa hatari zaidi wa kulinda amani nchini Afghanistan. Katika mahojiano na gazeti moja mjini Berlin, Berliner Zeitung, Struck amesema kuwa kuazia Oktoba jeshi la ulinzi la Ujerumani litatoa mafunzo kwa vikosi vya kupambana na madawa ya kulevya na kutoa msaada wa usafirishaji kama sehemu ya operesheni ya kijeshi la jeshi la kulinda amani la ISAF.

Kuhusu Sudan, waziri huyo amesema serikali ya Ujerumani iko tayari kupeleka jeshi lake iwapo ujumbe wa kulinda amani wa mataifa ya Afrika utashindwa. Ujerumani hata hivyo haitakuwa kiongozi wa ujumbe huo wa kulinda amani.