1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Je ndege iliyotekwanyara iaungushwe?

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPD

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amesema,katika hali ya hatari,ndege iliyotekwa nyara na magaidi kwa ajili ya kufanya mashambulizi,itapigwa na kuangushwa hata kama kuna abiria ndani ya ndege hiyo.Hatua hiyo hiyo itachukuliwa licha ya kutokuwepo msingi wa kisheria.

Waziri Jung,katika mahojiano yake na jarida la Kijerumani Focus alisema,ikiwa hakuna njia yo yote nyingine,atatoa amri ya kuiangusha ndege hiyo,ili umma uweze kulindwa.Akaongezea,ni matumaini yake kuwa serikali ya mseto itaweza kuafikiana kuhusu msingi wa kisheria.

Katika mwaka 2006,Mahakama ya Katiba ilipinga kile kilichoitwa sheria ya usalama wa anga, ikihusika na kuangusha ndege ya abiria iliyotekwa nyara.