BERLIN; Italia yatwaa kombe la dunia katika kandanda
10 Julai 2006
Italia imebeba kombea la dunia katika kandanda baada ya kuibwaga Ufaransa kwa penati mabao matano kwa matatu.
Hadi kumalizika muda wa nyongeza timu hizo zilikuwa zimefungana bao moja kwa moja.
Ufaransa ilianza kuliona lango la Italia kwa bao la penati iliyopigwa na mchezaji wake maarufu Zinedine Zedane mnamo dakika za mwanzo za pambano.
Italia ilisawazisha kwa goli la kichwa lililofungwa na Materrazi katika mpira wa kona kutoka kwa Andrea Pirlo.
Hatahivyo pambano hilo la fainali liliingia dosari ya baada mchezaji mahiri wa Ufaransa Zedane kumshambulia mchezaji wa Italia kwa kichwa, wakati zilipobakia dakika kumi kabla ya kumalizika kipindi cha pili cha muda wa nyongeza.
Timu ya Ufaransa ilidhoofika baada ya mchezaji huyo muhimu sana kupewa kadi nyekundu.
Watu wanaokadirwa bilioni moja waliitazama fainali hiyo kwenye televisheni duniani kote.