1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Iran yajiandaa kuanza kurutubisha madini ya uranium wiki ijayo

3 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEMF

Mwanadiplomasia wa Ulaya amesema Iran itaanza kurutubisha madini ya uranium katika kinu chake cha Isfahan kuanzia juma lijalo, licha ya shinikizo la Marekani na umoja wa Ulaya kusitisha shughuli zake zote za kinuklia. Huku serikali ya Tehran ikijiandaa kuanza kazi hiyo, Marekani imesema hatua hiyo inaipeleka Iran katika matatizo makubwa na itaitenga kutoka jamii ya kimataifa.

Russia kwa upande wake imependekeza kuiruhusu Iran kuendeleza shughuli za kinuklia ambazo sio hatari ikishirikiana na serikali ya Moscow. Iran inasema mpango wake wa nuklia ni wa matumizi ya kuzalisha umeme na imekataa shinikizo la umoja wa Ulaya kusitisha shughuli zake, ili kuzuia kufikishwa mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Rais Hugo Chavez wa Venezuela ameonya kwamba kuishtaki Iran kwa baraza la usalama kutauchocheza mzozo huo wa kimataifa.