1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. IG Metall kimefia muafaka wa ongezeko la mshahara.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4k

Chama kikuu cha wafanyakazi wa viwanda vya chuma nchini Ujerumani IG Metall kimefikia muafaka wa makubaliano ya mshahara na waajiri katika jimbo la kusini la Baden- Württemberg baada ya zaidi ya saa 20 za mazungumzo.

Makubaliano hayo yatawapa wafanyakazi wa jimbo hilo wa viwanda vinavyotumia vyuma na vya umeme ongezeko la asilimia 4.1 mara moja, pamoja na ongezeko la asilimia 1.7 katika muda wa mwaka mmoja ujao.

Chama hicho cha wafanyakazi kimekuwa kikihitaji ongezeko la asilimia 6.5 , wakati waajiri wamekuwa hapo kabla wakitoa ahadi ya asilimia 2.5.

Makubaliano hayo yanaepusha kitisho cha mgomo wa nchi nzima na wachunguzi wa mambo wanasema kuwa hali hiyo inaweza kuwa njia ya kupata makubaliano katika maeneo mengine nchini humo.