1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Idadi ya wasio na kazi nchini Ujerumani yaongezeka.

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEyi

Idadi ya wasio na kazi nchini Ujerumani imeongezeka kwa zaidi ya moja asilimia tangu mwaka mmoja uliopita.

Shirika la kazi la Ujerumani limeripoti kuwa asilimia 11.3 ya Wajerumani hawana kazi hadi Juni 2005, 1.1 zaidi kuliko ilivyokuwa Juni 2004.

Lakini ikilinganishwa na miezi iliyopita , idadi imepungua kwa asilimia ndogo, kutokana na mabadiliko ya majira.

Shirika hilo limeeleza matumaini yake, kwa sababu idadi ya vijana ambao hawana ajira imepungua kwa kiwango kikubwa.

Katika mwaka uliopita, serikali imetekeleza kile kinachofahamika kuwa ni mageuzi ya Hartz 4, ambapo ni kujaribu kuboresha soko la kazi nchini Ujerumani.