1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Hatima ya mateka nchini Afghanistan haijulikani

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeS

Hatima ya Mjerumani alietekwa nyara nchini Afghanistan,juma moja na nusu iliyopita,bado haijulikani.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani,kikundi maalum cha dharura, kinaendelea na juhudi za kupata uhuru wa mhandisi huyo wa Kijerumani.

Wakati huo huo wanamgambo wa Taliban waliowazuia raia 22 wa Korea ya Kusini wamesema,wanaipa serikali muda zaidi ili kumpatia nafasi mjumbe anaetoka Korea ya Kusini,kujiunga na majadiliano ya kuwaachilia huru mateka hao.Mjini Kabul,mjumbe wa Korea ya Kusini,anatarajiwa kushiriki katika majadiliano ya dharura pamoja na Rais wa Afghanistan,Hamid Karzai na majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani.

Mara kwa mara Wataliban wametishia kuwaua wafanyakazi hao wa kutoa misaada,iwapo serikali ya Afghanistan haitowaachilia huru waasi wanane walio jela.Hapo awali,wanamgambo wa Taliban waliipa serikali muda hadi Ijumaa mchana kutimiza madai yao.Mateka mmoja wa Korea ya Kusini ameshauliwa na wateka nyara hao.