1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Hakuna maafikiano kuhusu kiwango cha chini cha malipo

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqN

Serikali ya mseto ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani haikuweza kuafikiana kuhusu madai ya vyama vya wafanyakazi ya kuweka kiwango kimoja cha mshahara wa chini wa kulipwa kote nchini. Wahafidhina wa chama cha Merkel wamesema,kuweka kiwango kimoja cha mshahara nchini kote, kutapoteza nafasi za ajira.Lakini serikali ilikubali kuchukua hatua kali ili kukomesha mtindo wa kuajiri wafanyakazi kutoka nje kwa malipo madogo mno.Sheria ya miaka 10 iliyokuwa ikizuia makampuni ya ujenzi kuleta Ujerumani, wafanyakazi kutoka nje kwa malipo madogo,sasa itatumika katika sekta 12 zingine za viwanda.Wakati huo huo serikali imekubaliana kuongeza matumizi yake katika huduma za kuwatazama wagonjwa walio wazee na walemavu. Ujerumani ni miongoni mwa nchi chache katika Umoja wa Ulaya,ambayo haikuweka kiwango cha chini cha mshahara unaoruhusiwa kulipwa.