BERLIN : Familia yaomba kuachiliwa mateka
17 Machi 2007Mwanamme wa Iraq ambaye mke wake wa Kijerumani na mwanawe wa kiume wanashikiliwa mateka na wanamgambo wa Iraq amewasihi wateka nyara kuwaachilia huru.
Mohamed al – Tornachi ametowa ombi hilo akiwa pamoja na mkwe wake wa kike katika ukanda wa video wa lugha ya Kiarabu uliosambazwa kwenye mtandao na kutangazwa kwenye televisheni nchini Ujerumani.Hannelores Krause na mwanawe wa kiume Sinan walitoweka hapo tarehe 6 mwezi wa Februari.
Jumamosi iliopita kundi la waasi wa Iraq lililokuwa halijulikani huko nyuma limetishia kwenye ukanda wa video kumuuwa mama huyo na mwanawe venginevyo serikali ya Ujerumani inawaondowa wanajeshi wake kutoka Afghanistan,
Serikali ya Ujerumani imesema inakwenda mbio kuhakikisha watu hao wanaachiliwa huru lakini haitokubali kusalitiwa.