BERLIN: Dawa za kuongeza nguvu katika spoti zikatazwe
25 Mei 2007Matangazo
Waziri wa ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble amelihimiza bunge la Ujerumani kwa haraka lipitishe sheria ya kuzuia dawa za kuongeza nguvu katika spoti.Mwito huo umetolewa baada ya wanaspoti mashuhuri wa Kijerumani katika mbio za baiskkeli, Erik Zabel na Rolf Aldag kukiri kuwa walipokuwa wakishindana katika miaka ya ’90 walitumia dawa ya kuongeza nguvu iliyopigwa marufuku-EPO.Wakati huo huo madaktari wawili wa timu mbili kuu za mbio za baiskeli wamefukuzwa kazi na maabara ya Chuo Kikuu cha Freiburg,baada ya kukiri kuwa waliwapa dawa za kuzidisha nguvu wanaspoti wa mbio za baiskeli waliokuwa wakishughulikiwa na madaktari hao.