BERLIN: China yafuta ziara ya waziri Peer Steinbruck
16 Novemba 2007Matangazo
China imefuta ziara iliyopangwa kufanywa na Waziri wa Fedha wa Ujerumani mjini Beijing.Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Ujerumani,ziara ya Peer Steinbruck iliyotazamiwa kufanywa mwezi wa Desemba,imefutwa na China kwa sababu ya shughuli nyingi za Waziri mpya wa Fedha wa China,Xie Xuren.Uhusiano kati ya Ujerumani na China umekuwa na mvutano tangu Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel kumpokea kiongozi wa kibudha wa Tibet Dalai Lama,katika ofisi yake mjini Berlin hapo tarehe 23 Septemba.