Berlin. China na Ujerumani yataka azimio haraka dhidi ya Iran.
21 Machi 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa China Wen Jiabao wamekubaliana haja ya kuidhinisha haraka muswada wa azimio la umoja wa mataifa kuhusiana na mpango wa Iran wa kinuklia.
Kufuatia mazungumzo kwa njia ya simu, viongozi hao wawili wamesema ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuwa pamoja dhidi ya ukaidi wa Iran unaoendelea wa miito ya kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium.