1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. CDU yaidhinisha makubaliano na SPD.

14 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIa

Watendaji wa chama cha Kihafidhina nchini Ujerumani wameidhinisha makubaliano na chama cha Social Democrats ambayo yanasafisha njia kwa ajili ya muungano mkuu utakaounda serikali ya mseto.

Kiongozi wa chama hicho cha kihafidhina na kansela mteule Angela Merkel amewataka viongozi wa chama kuunga mkono makubaliano hayo, ambayo yamefikiwa siku ya Ijumaa baada ya wiki kadha za majadiliano.

Hapo mapema viongozi wa chama cha SPD wameashiria uungaji wao mkono wa makubaliano hayo ya muungano. Vyama hivyo vinatarajiwa kufanya mikutano baadaye wiki hii , ambapo makubaliano hayo yanatarajiwa kuidhinishwa kwa kupata uungaji mkono wa wanachama wa vyama hivyo.

Chama cha SPD pia kinatarajia kumchagua kiongozi wao mpya wa chama , huku waziri mkuu wa jimbo la Brandenburg Matthias Platzeck akitarajiwa kushinda.