1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Bunge laidhinisha muda zaidi wa jeshi la Ujerumani Darfur.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6U

Bunge la Ujerumani kwa wingi mkubwa leo Ijumaa limerefusha muda wa ujumbe wa kijeshi wa nchi hiyo ulioko katika jimbo la Darfur nchini Sudan kwa muda wa miezi sita hadi Novemba.

Wabunge wa Bundestag kutoka vyama vyote vikuu walizungumzia dhidi ya uvunjwaji wa haki za binadamu katika jimbo hilo la magharibi ya Sudan.

Wazungumzaji waliizungumzia ripoti ya umoja wa mataifa kuwa serikali ya Sudan ilikuwa ikitumia ndege za kubeba abiria kuwa ni ndege za umoja wa mataifa na kusafirisha silaha ndani ya jimbo hilo.

Kiasi cha wanajeshi 75 wa Ujerumani wanashiriki katika ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan.