Berlin. Bunge la Bundesrat larefusha muda wa jeshi la kulinda amani la Ujerumani katika jimbo la Kosovo.
22 Juni 2007Baraza la wawakilishi la bunge la Ujerumani limepiga kura kurefusha muda wa kikosi cha kulinda amani cha jeshi la Ujerumani Bundeswehr katika jimbo la Serbia la Kosovo kwa mwaka mmoja zaidi.
Ujerumani ina idadi kubwa ya wanajeshi katika jeshi la kulinda amani la KFOR, likiwa na wanajeshi 2,200 walioko karibu na Prizren.
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Russia kukataa muswada wa azimio juu ya hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Muswada huo wa azimio ungewapatia viongozi wa Kiserb na wale wenye asili ya Albania katika jimbo la Kosovo siku 120 za majadiliano zaidi.
Russia imepinga kipengee ambacho chini yake Kosovo ingepewa uhuru mwishoni mwa miezi hiyo minne iwapo hakutakuwa na makubaliano yaliyofikiwa.