BERLIN : Bunge kuidhinisha vikosi vya Ujerumani kwa Lebanon
20 Septemba 2006Matangazo
Bunge la Ujerumani linatarajiwa kupiga kura kwa wingi leo hii kuidhinisha upelekaji wa vikosi vya Ujerumani nchini Lebanon.
Juu ya kwamba shughuli hizo za kulinda amani zinaelezewa kuwa za kihistoria na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kura huyo itapigwa huku kukiwa na ongezeko la mashaka ya wananchi juu dhima za shughuli hizo za kulinda amani nchi za nje.
Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba idadi kubwa ya Wajerumani wanapinga shughuli hizo za kulinda amani Mashariki ya Kati ambapo kwayo serikali ya Ujeruamni itachangia wanajeshi hadi 2,400 wanamaji na wale wa anga kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kitakachokuwa na jukumu la kusimamia usitishaji wa mapigano kati ya Israel na wapiganaji wa Hizbollah nchini Lebanon.