1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Bibi Angela Merkel kupimana nguvu na kansela Gerhard Schröder.

31 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8N

Vyama vya upinzani vimeafikiana kumpitisha bibi Angela Merkel kuwa mgombea kiti cha kansella katika uchaguzi mkuu ujao wa Ujerumani.

Bibi Merkel ambae ni mwenyekiti cha Christian Democartic Union CDU huenda akawa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika historia ya Ujerumani.

Uchaguzi mkuu ujao nchini Ujerumani unatarajiwa kufanyika mwezi septemba ambako bibi Merkel atajibwaga uwanjani kushindana na kansela Gerhard Schröeder.

Kansela Gerhard Shröeder wa Ujerumani ameitisha uchaguzi mkuu wa mapema baada ya chama chake cha SDP kushindwa vibaya katika uchaguzi wa mikoa.

Kura ya maoni tangu wiki iliyopita kwa mara ya kwanza imeonyesha kuwa bibi Merkel yuko mbele ya kansela Gerhard Schröeder.