1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Bibi Angela Merkel atoa wito kupunguzwa gesi za viwandani.

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByi

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel ametoa mwito wa kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi zinazotolewa viwandani zinazoathiri hali ya hewa.

Bibi Angela Merkel amesema hana hakika iwapo mkutano wa mwezi ujao wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, utasaidia kwa vyovyote vile kupatikana makubaliano ya kudhibiti hali-joto duniani.

Bibi Angela Merkel atakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaokuwa mjini Heiligendamm kuanzia tarehe sita mwezi ujao unaotarajiwa kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo barani Afrika na pia ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa.

Kansela huyo wa Ujerumani amekuwa akikabiliwa na upinzani hasa kutoka Marekani kwa nia yake ya kuwasilisha katika kikao hicho mkataba wa Kyoto unaoshugulikia mazingira.

Bibi Angela Merkel ametoa wito waandamanaji waliopanga kuhudhuria mkutano huo, kuandamana kwa amani.