1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Bibi Angela Merkel ahutubia wabunge wa Ujerumani.

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByp

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel anayetarajiwa kuwa mwenye wa mkutano wa mwezi ujao wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, amesema maafikiano yatapatikana hatimaye kuhusu mashauriano yaliyokwama ya Doha ya kuweka huru biashara ya dunia.

Bibi Angela Merkel amewaambia wabunge wa Ujerumani suitafahamu iliyoko inaweza kuondolewa iwapo makundi yote husika yataridhia makubaliano.

Kuhusu maandalizi ya kiusalama katika mkutano wa G8 Kansela huyo wa Ujerumani amesema:

"Nasema, anayetumia mabavu anakorofisha majadiliano. Ninasema bayana kwamba hao wanaopinga hatua za kuweka usalama katika mkutano huo ndio watakaokuwa wa kwanza kulaumu maafisa wa usalama iwapo ghasia zitazuka.

Vinginevyo ni wazi kwamba watakaoandamana kwa amani, madai yao sio tu yanakubalika lakini pia tutayazingatia"

Kwa mujibu wa Bibi Merkel endapo mataifa yatakubaliana kuhusu kuweka huru biashara ya kimataifa, vizingiti vingi vitaondolewa na hivyo kuyasaidia mataifa maskini.