1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Baraza la mawaziri laidhinisha kurefusha muda wa jeshi la Ujerumani.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOP

Serikali ya Ujerumani imeidhinisha urefushwaji wa muda wa operesheni mbili za kijeshi nchini Afghanistan. Mjini Berlin , baraza la mawaziri la kansela Angela Merkel limepiga kura kurefusha kwa mwaka mmoja muda wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr katika jeshi la kimataifa la linalosaidia kulinda amani pamoja na uwekaji wa ndege za uchunguzi nchini Afghanistan.

Kwa hivi sasa kiasi cha wanajeshi 3,000 wa Ujerumani wako nchini Afghanistan. Mjadala mkubwa unatarajiwa kuanza kesho Alhamis na kura ya mwisho itapigwa mwezi Oktoba.