1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Bado hakuna makubaliano juu ya mgomo wa reli

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKC

Inaonekana kwamba hakuna suluhisho la karibuni katika usafiri wa reli nchini Ujerumani.

Mgomo wa masaa 42 wa madereva wa treni umemalizika ambapo treni 1,300 za mizigo zilishindwa kutowa huduma.Eneo la mashariki mwa Ujerumani ndio lililoathirika zaidi kwa takriban kusita kwa huduma zote za treni za mizigo.

Msemaji wa chama cha wafanyakazi madereva wa treni nchini GDL amesema migomo zaidi ya kazi inaweza kufanyika wiki ijayo.

Shirika la reli la taifa Deutsche Bahn limesema kwamba migomo hiyo imekuwa ikahatarisha ajira kadhaa katika shirika hilo.