1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bensouda ateuliwa kuongoza uchunguzi Ethiopia

3 Machi 2022

Mwendesha mashitaka mkuu wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai - ICC ataongoza uchunguzi kuhusu madai makubwa ya ukiukaji uliofanywa na pande zote katika mzozo wa Ethiopia.

https://p.dw.com/p/47wTZ
Fatou Bom Bensouda
Picha: CC BY-SA 3.0

Fatou Bensouda wa Gambia, aliyehudumu kama mwendesha mashitaka mkuu wa ICC kuanzia 2012 hadi 2021, ni miongoni mwa watalaamu watatu wa kimataifa walioteuliwa na rais wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza hali ya haki za binaadamu nchini Ethiopia. 

Rais wa Baraza hilo Balozi Federico Villegas wa Argentina, pia amemteuwa Kaari Betty Murungi wa Kenya na Steven Ratner wa Marekani kuhudumu kwenye Tume hiyo mpya ya Kimataifa.

Tume hiyo iliundwa ya Wataalamu wa Haki za Binaadamu nchini Ethiopia. 

Chanzo: ap