1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Ufaransa Sociate Generale yakiri ilishindwa kugundua wizi wa mabilioini ya pesa.

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyhQ

PARIS:

Benki ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa-Societe Generale, imekiri kuwa mfumo wake wa ulinzi dhidi ya mgogoro ulishindwa kugundua hasara ya Euro billion tano –ambazo ni sawa na dola billioni 7.Katika taarifa iliotolewa,benki imesema kuwa mtumishi wake wa ngazi ya chini -Jerome Kerviel -alikwepa mfumo huo wa ulinzi kwa kuunda akaunti bandia.Benki hiyo imemfungulia mashtaka Kerviel,ambae alijisalimisha kwa polisi mwishoni mwa juma.Wendesha mashtaka wanaishughulikia kesi kubwa ya udanganyifu kuwahi kutokea nchini humo.Aidha watamfungulia mashtaka Kerviel ama kumuachilia huru kutoka kituo cha polisi anakozuiliwa sasa. Wakili wa Kerviel anasema mteja wake hata hatia, na kuwa hakufaidika na mali ya benki.