1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki kuu duniani zaingilia kati mzozo wa fedha

Kalyango Siraj18 Septemba 2008

Juma moja zimetumiwa dola zaidi ya billioni 600

https://p.dw.com/p/FKtq
Soko la hisa la New York MarekaniPicha: AP

Mzozo katika masoko ya fedha ya kimataifa baado unaendelea licha ya hatua kadha kuchukuliwa na benki kuu ya Marekani ya kuongeza dola zaidi kwa lengo la kuokoa jahazi la kiuchumi ambalo linaonekana linataka kuzama.

Hali hiyo imepelekea benki kuu kadhaa kuweka pesa zaidi ya dola billioni 300 ili kusaidia uwezekano wa kuporomoka kwa masoko ya fedha.

Benki kuu muhimu na mashuhuri duniani zimejitokeza ili kuweza kuokoa uchumi unaoyumbayumba.

Benki hizo zimetoa kwa jumla kitita cha dola billioni kadhaa katika soko kama kupiga jeki uchumi unaoyumbayumba.

Katika hali ambayo haikutegemewa,benki kuu ya Marekani imetoa donge lingine nono la ziada ili kuzisaidia benki kuu zingine duniani katika juhudi za kuokoa jahazi la uchumi linalokwenda mrama.

Donge hilo ni la dola za kimarekani billioni 180. Miongoni mwa benki kuu zingine zilizoingilia kati kunusuru mgogoro wa fedha ni kama vile benki kuu za Japan,Kanada,Umoja wa Ulaya pamoja na ya Uingereza.

Mwandishi wa habari Suleiman Salim akiwa London anasema hatua hiyo inachekesha na kushangaza.

Mbali na hatua za kuokoa lakini baado wasiwasi ulikuwa umetanda katika ulimwengu wa soko la fedha.Bei za hisa zilishuka vibaya barani asia,na bei ya dhahabu ikapanda wakati wenye wafanya biashara wakijaribu kunuru rasli mali zao.Kutokana na hali hiyo sarafu y Euro inayotumiwa barani Ulaya ilipanda thamani zaidi ya senti moja dhidi ya sarafu ya dola.

Hekaheka hizi za kuunusuru uchumi unaoyumbayumba umezifanya benki kuu kuwa, katika kipindi cha wiki hii moja tu, zimetumia dola zaidi ya billioni 600 katika juhudi hizo.

Miongoni mwa juhudi zingine zilizochukuliwa kuokoa jahazi ni kushudia benki kadhaa mashuri duani kuunganishwa pamoja.Mfano nchini Uingereza, benki ya Lloyds TSB imeichukua ile ya Halifax Bank of Scotland HBOS.

Na hapa Ujerumani kumetokea mgogoro mwingie ambapo inasemekana benki moja ya kijerumani ilihamisha mamilioni ya Euro karibu millioni 300 katika benki ya Marekani ilifilisika ya Lehman Brothers kabla ya kufilisika.Inasemekana kuwa malipo hayo ni sehemu ya mktaba wa mda mrefu lakini yameikasirisha serikali ya Berlin kiasi kwamba imeamuru kufanyika uchunguzi wa kina.Hii ni kuwa kisheria benki hiyo inayodhaminiwa na serikali ya KfW haipaswi kuhamisha pesa hadi kampuni yoyote inayofilisika.

Na haijulikani ikiwa Euro millioni 300 za walipa kodi wa hapa Ujerumani zitaokolewa.