1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benedikt wa 16 ziarani nchini Brazil

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2s

Sao Paulo:

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwengui Benedikt wa 16 akiwa ziarani nchini Brazil amelalamika dhidi ya waumini wanaozidi kulipa kisogo kanisa katoliki katika eneo la latin Amerika.“Hili ni tatizo kubwa „ amesema kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni,wakati wa mazungumzo pamoja na maaskofu wa Brazil mjini Sao Paulo.Wakati huo huo Papa Benedikt wa 16 amewatuhumu waprotestanti na makundi mengineyo ya kikristo „kuwashawishi wakatoliki.“Kabla ya hapo kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni aliongoza misa ya hadhara wakihudhuria zaidi ya waumini milioni moja.