1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belgrade: Maandamano Serbia kuupinga mpango wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kosovo

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CBHR

Maelfu ya waandamanaji wa Ki-Serbia wamekusanyika nje ya jengo la ubalozi wa Marekani mjini Belgrade wakiupinga mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya baadae ya jimbo la Kosovo lilolijitenga. Mpango wa Umoja wa Mataifa unawapa Wa-Albania wenye asili ya Kosovo ambao ni wengi katika jimbo hilo aina ya dola, lakini sio ilio huru kamili.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya mzozo wa Kosovo, Marrti Ahtisaari, ambaye alitoa mapendekezo yake karibuni, amesema:

+Ni wazi kwamba katika suala la hali ya baadae, ni shida kufikiria kwamba watu watabadilisha maoni yao, na hiyo ndio maana nitatoa mapendekezo yangu mwishoni mwa mwenendo huu.+

Baraza la taifa la Serbia ambalo limeandaa maandamanao hayo lilisema yamefanywa mbele ya ubalozi wa Marekani kwa vile nchi hiyo inawaunga mkono wa-Albania wenye kudai uhuru kwa Kosovo.