BEJING:Marekani yataka mzozo wa mpango wa nuklia wa Korea Kusini umalizwe haraka
22 Januari 2007Kiongozi wa Marekani katika mazungumzo juu ya mzozo wa mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini, Christopher Hill amesema kuwa ni lazima makubaliano yafikiwe haraka iwezekanavyo.
Alisema hayo baada ya kukutana na mjumbe wa China kwenye mazungumzo hayo Wu Dawei mjini Beijing, kabla ya kurejea Washington.
Hill pia alikuwa na mazungumzo na viongozi wa Japan, Korea Kusini, ambapo pia alikutana na mwakilishi wa Korea Kskazini katika mazungumzo hayo, Kim Kye-Gwan.
Mjumbe huyo wa Marekani amesema kuwa China hivi karibuni inatarajiwa kutangaza tarehe ya kurejewa tena kwa mazungumzo ya mataifa sita juu ya mzozo huo wa mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini.
Mjini Pyongyang, shirika la habari la Korea Kaskazini, limearifu kuwa China inatarajiwa kutangaza tarehe ya kurejewa tena kwa mazungumzo hayo leo au kesho.
China imekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya pande sita kuhusiana na mzozo huo.