BEIRUT:Waziri mkuu wa Lebanon alaani mashambulio ya mábomu nchini humo
23 Julai 2005Waziri mkuu wa Lebanon Fouad al Siniora amelaani mashambulio ya mabomu ya hapo jana nchini humo na kuyajata kuwa yaliyodhamiriwa kuitatiza serikali mpya.
Watu kumi na mbili walijeruhiwa katika miripuko ya mabomu mjini Lebanon.
Mkurugenzi mkuu wa masuala ya usalama wa ndani nchini Lebanon,Generali Ashraf Rifi alikiambia kituo cha televisheni cha Lebanon kwamba magari mawili yalitekeketea baada ya mabomu yaliokuwa yametegwa ndani ya magari hayo kuripuka.
Taarifa za awali ziliarifu mtu mmoja ameuwawa kwenye miripuko hiyoo.
Miripuko hiyo imefanyika katika barabara yenye shughuli nyingi za kibiashara katika eneo linalokaliwa na wakrito wengi mashariki ya mji wa Beirut, saa chache baada ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice hapo jana.