BEIRUT:Washirika wa Syria waelekea kushinda uchaguzi nchini Lebanon
13 Juni 2005Matangazo
Katika duru ya tatu ya uchaguzi nchini Lebanon wagombea wanaoiunga mkono serikali ya Syria wanaelekea kupata ushindi mkubwa.
Wagombea hao wanaoongozwa na kamanda wa zamani wa jeshi nchini humo, Michael Aoun wanaongoza katika uchaguzi huo katika wilaya muhimu nchini humo.
Uchaguzi kama huo pia umefanyika katika jimbo la Bekaa.Takriban nusu ya viti 128 vilikuwa vinagombewa .Uchaguzi huo ndio wa kwanza kufanyika nchini Lebanon bila kuwepo wanajeshi wa Syria.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa baadae leo hii.