BEIRUT:Wanajeshi wa Marekani wameingia Lebanon kuwaondoa raia wao
20 Julai 2006Matangazo
Kiasi wanajeshi 40 wa Marekani wameingia nchini Lebanon kwa ajili ya opresheni ya kuwaodoa raia wake na raia wengine wakigeni walioko nchini humo.
Rais Bush amezungumzia juu ya mashambulio yanayofanywa na Israel akigusia kwamba nchi yake iko pamoja na Israel.Anasema
’’Nautaka ulimwengu kuangalia chanzo hasa cha matatizo haya.Kwa kweli sababu kubwa ni kundi la Hezbollah na sisi tumeshikamana na Israel japo hatuwezi kuiambia nchi hiyo namna ya kujilinda kutokana na mashambulio ya Hezbollah lakini tunaitolea mwito wa kujitahadhari.’’
Raia wapatao 1000 wa Marekani waliwasili hapo jana huko Cyprus wakitokea Beirut ambako mashambulio ya Israel yamechacha.
Mabasi hamsini yamekodiwa kuwahamisha kiasi wajerumani elfu 3 waliokuwasanyika mjini Beirut.Wajerumani hao watapelekwa mjini Damscus nchini Syria na kutoka huko watarejeshwa nyumbani