1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Risasi zimefyatuliwa kwenye mpaka wa Lebanon na Israel

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCU2

Vikosi vya Lebanon na Israel vimefyatuliana risasi kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.Kwa mujibu wa jeshi la Lebanon,wanajeshi wake walilifyatulia risasi buldoza la Waisraeli ambalo lilivuka mpaka uliowekwa na Umoja wa Mataifa.Vikosi vya Kiisraeli vilivyo upande wa pili wa mpaka vikajibu risasi hizo.Waisraeli wamesema,wanajeshi wake mpakani,walikuwa wakisaka miripuko iliyofichwa na wanamgambo wa Hezbollah.Tangu mwaka jana,hii ni mara ya kwanza kwa vikosi hivyo kubadilishana risasi,baada ya kumalizika kwa vita vya mwezi mmoja kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.