Beirut:Misaada ya dharura kupelekwa Lebanon.
24 Julai 2006Mratibu mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland ametembelea sehemu ya mpakani kusini mwa Beirut iliyoharibiwa kutokana na mashambulizi ya mabomu ya Israel.
Amesema, Israel imekuwa ikiripua maeneo ya miundo mbinu ya raia, lakini pia amewalaumu Hezbollah kwa kurusha maroketi huko Israel, huku akisema kuwa ni vita visivyo na maana kwa pande zote mbili.
Watu wengine zaidi ya maelfu wameelekea Cyprus na Uturuki, na kiasi ya meli 15 zinategemewa kuwasili katika bandari ya Cyprus hii leo kuchukua raia wao, wengi wao wakiwa ni wa-faransa, wa-canada na wa- marekani.
Akizungumzia kuhusu kutoa misaada kwa wananchi wa Lebanon Jan Egeland amesema: Siku chache zijazo Umoja wa Mataifa utatuma gari zake za misaada, ambazo zitakuwa na vitu vyote viinayohusu misaada ya raia, lakini akasisitiza vitendea kazi na usalama kwa vitu vyao na hata gari watakazo tumia.