1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Mashambulizi zaidi yafanywa na Israel huko Lebanon.

8 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDNZ

Ndege za kivita za Israel zimeendeleza mashambulizi yake kusini mwa Beirut na kuuwa watu kiasi ya wanane na kujeruhiwa kadhaa.

Mapema mashambulizi ya anga ya Israel yaliuwa kiasi cha watu saba karibu na Sidon, mji wa kusini wa Lebanon.

Wakati huo huo Waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora amesawazisha lawama za awali kwamba ndege za Israel ziliuwa watu 40 katika kijiji cha Hula.

Jeshi la Israel limesema limepoteza wanajeshi wake watatu huko kusini mwa Lebanon katika kijiji cha Bint Jbeil, wakati wanamgambo watano wa Hezbollah wameuliwa katika kijiji hicho.

Jeshi la Israel limeongeza kuwa, limeitungua ndege ya Hezbollah isiyokuwa na rubani.

Hezbollah nao walirusha maroketi zaidi ya 160 huko kaskazini mwa Israel hapo jana na kujeruhi watu watatu.